1 Peter 4

1Kwa hiyo, kwa kuwa Kristo aliteseka katika mwili, jivikeni silaha za nia ile ile. Yeye aliyeteseka katika mwili ameondokana na dhambi. 2Mtu huyu haendelei tena kuishi katika tamaa za mwili, bali kwa mapenzi ya Mungu, kwa maisha yake yaliyosalia.

3Kwa kuwa muda uliopita umetosha kutenda mambo ambayo wamataifa wanataka kufanya- ufisadi, nia mbaya, ulevi, ulafi, sherehe za kipagani na ibada za sanamu zenye machukizo. 4Wanafikiri ni ajabu mnapojiepusha kutenda mambo hayo pamoja nao, hivyo wananena maovu juu yenu. 5Watatoa hesabu kwake aliye tayari kuhukumu walio hai na wafu. 6Kwa kusudi hili injili ilihubiriwa kwao waliokwisha kufa, kwamba ijapokuwa walikwisha hukumiwa katika miili yao kama wanadamu, ili waweze kuishi kulingana na Mungu katika roho.

7Mwisho wa mambo yote unakuja. Kwa hiyo, mwe na ufahamu ulio sahihi, na iweni na nia njema kwa ajili ya maombi yenu. 8Kabla ya mambo yote, eweni na bidii katika upendo kwa kila mmoja, kwa kuwa upendo hautafuti kufunua dhambi za wengine. 9Onyesheni ukarimu kwa kila mmoja bila kunung’unika.

10Kama ambavyo kila mmoja wenu alivyopokea karama, itumieni katika kuhudumiana, kama wasimamizi wema wa karama nyingi zilizotolewa bure na Mungu. 11Kama mtu akiongea, na iwe kama mausia ya Mungu, na kama mtu akihudumu, na iwe kama uwezo aliopewa na Mungu, ili kwamba kwa kila jambo Mungu apate kutukuzwa kupitia Yesu Kristo. Utukufu na uweza vina Yeye milele na milele. Amina.

12Wapendwa, msihesabu jaribu ambalo huja kuwajaribu kama kitu kigeni, ingawa kuna kitu kigeni kilichokuwa kinatukia kwenu. 13Lakini kwa kadri mnavyozidi kupata uzoefu wa mateso ya Kristo, furahini, ili kwamba mfurahi pia na kushangilia katika ufunuo wa utukufu wake. 14Iwapo mmetukanwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu ya Roho wa utukufu na Roho wa Mungu anakaa juu yenu.

15Lakini asiwepo yeyote mwenye kuteswa kama muuaji, mwizi, mtenda maovu, au ajishughulishaye na mambo ya wengine. 16Lakini ikiwa mtu anateswa kama Mkristo, asione aibu, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.

17Kwa kuwa wakati umefika kwa hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Na kama inaanzia kwetu, itakuwaje kwa wale wasioitii injili ya Mungu? 18Na kama “mwenye haki anaokolewa kupitia magumu, itakuwaje kwa mtu asiyehaki na mwenye dhambi?” Kwa hiyo wote wanaoteseka kutokana na mapenzi ya Mungu wakabidhi nafsi zao kwa Muumba mwaminifu ili hali wakitenda mema.

19

Copyright information for SwaULB